Balozi
wa Japan Tanzania, Masaki Okada, amesema uhusiano wa kibiashara kati ya
Tanzania na Japan unazidi kuwa mzuri na kielelezo kimojawapo ni kampuni zaidi
kutoka nchini kwake kufungua shughuli zake jijini Dar es Salaam.
Amesema
hayo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa ofisi za kampuni ya Samurai
Japan Trading Limited inayojihusisha na uuzaji wa magari.
Akizungumza
kwenye tukio hilo, Mkurugenzi wa Utafiti wa Uchumi na Sera wa Benki Kuu ya
Tanzania (BoT), Dk. Joseph Massawe, amewataka Wajapani kuwekeza nchini kwa
sababu kuna fursa nyingi za uwekezaji na uchumi unaokua.
Amesema
kiuchumi nchi iko sehemu nzuri kati ya nchi za Kiafrika jambo ambalo
litawasaidia kupanua biashara yao
No comments:
Post a Comment