GHAZA
Mtoto mchanga wa Kipalestina na
watu wazima wanne wameuawa shahidi katika mashambulizi ya ndege za kivita za
Israel huko kaskazini na katikati mwa Ukanda wa Ghaza.
Mashambulizi hayo ya Wazayuni ni
ukiukaji wa makubaliano ya muda ya usitishaji vita yaliyosainiwa siku sita
zilizopita kati ya utawala huo na ujumbe wa Palestina kwenye mazungumzo huko
Cairo Misri.
Wapalestina wengine zaidi ya 12
wamejeruhiwa katika mashambulio hayo ya ndege za kivita za Tel Aviv katika
maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Ghaza.
Jeshi la Israel limedai kuwa
Wapalestina wamerusha makombora kadhaa yaliyotua huko kusini mwa Israel.
Weledi wa mambo wanasema kuwa
Israel inaendeleza mashambulizi yake huko Ghaza ili kuzidi kuwashinikiza
wajumbe wa Palestina wakubali kusaini makubaliano ya kudumu ya usitishaji vita
bila ya kukidhiwa matakwa yao.
Baada ya kujiri mashambulizi hayo
ya Israel, harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas pia imeanzisha
mashambulizi ya makombora kuelekea Israel baada ya utawala huo kukiuka
makubaliano ya kusimamisha vita huko Ghaza.
No comments:
Post a Comment