PWANI
Ukosefu wa uwazi,
uwajibikaji na ukiukwaji wa haki za binadamu katika maeneo mbali mbali ya kazi
huchangia kwa kiasi kikubwa kukosekana kwa utawala bora.
Hayo yameelezwa
mjini Kibaha na muwezeshaji, Bumija Senkondo, katika semina ya kuinua ufahamu
wa wanachama na viongozi wa kikundi cha Ushirikiano wa Wanawake Kibaha (Uwaki),
kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kuongoza asasi za kiraia.
Senkondo amesema
sehemu yeyote inayokosa uwazi suala la kuminya haki za binadamu litajitokeza na
kwamba hali hiyo inachangiwa na kukiukwa kwa misingi ya uongozi wa taasisi
yoyote iliyokubaliwa kufuatwa na washirika.
Amesema katika
ushirika wa aina yoyote ni vyema wahusika wakajitolea kuhakikisha wanatimiza
malengo waliyojipangia badala ya kufikiria kunufaika kwa muda mfupi.
Naye Hamis Masasa,
akitoa mada ya namna ya kuandaa mpango kazi wa kufikia malengo yaliyokusudiwa,
ameeleza kuwa ni wajibu wa washirika kuwa na maono ya wapi wanataka kuwa baada
ya miaka mitano kutoka sasa.
Amesema kama
hawatakuwa na malengo ya wapi wanakusudia kufika baada ya muda waliojiwekea
umoja wao hautakuwa na maana yoyote katika kuwaletea mabadiliko
No comments:
Post a Comment