MOGADISHU
Vikosi vya usalama vya Somalia
vimemtia mbaroni mmoja wa viongozi wa maharamia wa nchi hiyo, ambaye anadaiwa
kuziteka nyara meli kubwa katika pwani ya Somalia.
Kiongozi huyo wa maharamia wa
Somalia amekuwa akijipatia mamilioni ya dola kupitia fedha alizokuwa akilipwa
kama kikomboleo.
Duru za usalama za nje na za ndani
ya Somalia zimetangaza kuwa vikosi vya usalama vya Somalia vimemtia mbaroni
Mohamed Garfanji pamoja na walinzi wake kadhaa huko Mogadishu mji mkuu wa nchi
hiyo.
Rais Hassan Sheikh
Mahmoud wa Somalia mwaka jana alitoa msamaha kwa maharamia wa nchi hiyo
ili kukomesha mashambulizi yao karibu na pwani ya nchi hiyo ya eneo la Pembe ya
Afrika, hata hivyo alisema kuwa msamaha huo hauwahusu viongozi wa mtandao
huo.
Imeelezwa kuwa Mohamed Garfanji
amekamatwa katika oparesheni moja ya upokonyaji silaha na kwamba ametiwa
mbaroni si kwa sababu ya uharamia.
No comments:
Post a Comment