DAR
ES SALAAM
Serikali
kwa kushirikiana na wadau wa sekta binafsi ya miundombinu ya reli na barabara
inatarajia kufanya maboresho ya usafiri wa reli ya kati na Uwanja wa Ndege wa Mwalimu
Julius Nyerere
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Shaaban Mwinjaka, ameyasema hayo kwenye mkutano
uliowashirikisha wadau mbalimbali wa miundombinu jijini Dar es Salaam.
Amesema
Serikali ipo katika mikakati madhubuti ya kuhakikisha huduma ya usafiri wa reli,
barabara na anga unaimarika.
Ameongeza
kuwa Serikali inatarajia kupokea mabehewa 400 na vichwa 50 vya treni kwa
ajili ya uboreshaji wa usafiri wa Jiji la Dar es Salaam.
Aidha,
amesema Serikali ina mpango wa kuanzisha usafiri wa treni kutoka Dar es Salaam
kwenda Mkuranga, mkoani Pwani.
Amesema
usafiri wa treni unaendelea kuboreshwa hasa kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro.
No comments:
Post a Comment