Tuesday, August 19, 2014

MOHAMMED ABOUTREKA AKATAA KUCHEZA MECHI YA KULETA AMANI NA MCHEZAJI WA KIYAHUDI





Gwiji wa Soka nchini Misri, Mohamed Aboutreka anayesifika kwa ucha mungu na tabia njema amekataa mualiko wa Vatican kwa ajili ya mechi ya kuleta amani katika ukanda wa Ghaza

Aboutreka ametoa taarifa ya kukataa mualiko huo katika Akaunti yake ya Twitter kwa kusema kuwa hawezi kushiriki pamoja na mchezaji wa kiyahudi, akimaanisha ushiriki wa mchezaji wa kiisrael Yossi Benayoun.

Mechi hiyo imeandaliwa na 'Pontifical Academy for Social Science and the Pupi Foundation' inayomilikiwa na Gwiji wa zamani wa Intermilan Javier “Pupi” Zanetti na makao makuu yake yapo Buenos Aires. 




Mechi hiyo itakayo washirikisha wachezaji nyota duniani wa dini mbalimbali, imepokea mchango mkubwa kutoka kwa Papa Francis na Vatican ili kufanikisha.

Baadhi ya Wachezaji wanaotarajiwa kushiriki ni Robert Baggio ambaye ni Buddha, Mchezaji wa zamani wa Chelsea Yosi Benayoun Myahudi na Zinedine Zidane Muislamu.
Nyota wa Barcelona Lionel Messi na aliyekuwa mshambuliaji wa Chelsea Samuel Eto'o wanatarajiwa kucheza mechi hiyo ambayo inatarajiwa kuchezwa Septemba mosi 2014 mjini Rome, Italia.
Ikumbukwe kuwa, Aboutreka ni Balozi wa mpango wa kuondoa njaa Duniani wa World Food Program.






No comments:

Post a Comment