Serikali imeanza kutoa fomu maalum za kuhoji
wasafiri zinazotumika katika viwanja vya ndege vya kimataifa vya Mwalimu Julius
Nyerere na cha Kilimanjaro ikiwa ni katika tahadhari ya kukabiliana na Ugonjwa
hatari wa Ebola.
Mbali na hilo serikali imeunda kikosi kazi
kinachohusisha wajumbe mbalimbali wakiwemo wadau wa maendeleo, Shirika la Afya
Duniani (WHO), UNICEF, USAID na watendaji wengine kutoka taasisi za WAUJ katika
mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar
es Salaam, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid amesema kuwa fomu
hizo maalum zinatumika katika viwanja hivyo na maeneo yote maalum ikiwemo
mipakani.
Amesema pia wameanza kuwatambua abiria
wanaoingia nchini na kuainisha nchi walizotoka kabla ya ndege kutua.
Dk. Rashid amesema kuwa serikali pia imeagiza
‘Thermoscanners’ zitakazowekwa katika viwanja hivyo ili kurahisisha utambuzi wa
wasafiri watakaorudi na dalili za mwanzo ambayo ni homa.
No comments:
Post a Comment