Saturday, August 9, 2014

TAARIFA YA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA (ACSEE) ULIOFANYIKA MEI 2014




1.    UTANGULIZI
Baraza la Mitihani la Tanzania katika kikao chake cha 100 kilichofanyika tarehe 15 Julai, 2014liliidhinisha kutangazwa rasmi kwa matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) uliofanyika tarehe 05 – 21 Mei 2014. Matokeo haya yamechakatwa kwa kutumia viwango vya alama na madaraja ya ufaulu kama ilivyooneshwa katika Jedwali la 1 na la 2.

Jedwali la 1: Viwango vya Ufaulu.

Alama
Uwigo wa Alama
A
75 – 100
B+
60 – 74
B
50 – 59
C
40 – 49
D
30 – 39
E
20 – 29
F
0 – 19

 .Mtahiniwa atahesabiwa kuwa amefaulu somo endapo atakuwa amepata angalau gredi D (alama 30) katika somo husika. Hivyo, kiwango cha juu cha ufaulu katika somo ni Gredi A ambapo kiwango cha chini cha ufaulu (pass) katika somo ni Gredi D. Ufaulu katika gredi A, B+, B na C utakuwa ni ‘Principal Pass’.

Jedwali la 2: Madaraja ya Ufaulu.


DARAJA
POINTI/VIGEZO
I
3 – 7
II
8 – 9
III
10- 13
IV
Awe na angalau D mbili au ‘principal pass’moja isiyopungua C.
O
Aliyepata ufaulu chini ya D mbili


Uzito wa alama katika Gredi; A=1, B+= 2, B=3, C=4, D=5, E=6 na F=7.
2.    USAJILI NA MAHUDHURIO
1.    Watahiniwa wote 
Jumla ya watahiniwa 41,968 waliandikishwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita 2014 wakiwemo wasichana 12,674 (30.20%) na wavulana 29,294 (69.80%). Watahiniwa wa Shule walikuwa 35,650 ikilinganishwa na watahiniwa 43,231 walioandikishwa kufanya mtihani huo mwaka 2013.

Kati ya watahiniwa 41,968 waliosajiliwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita Mei 2014, watahiniwa 40,695 sawa na asilimia 96.97 walifanya mtihani na watahiniwa 1,273 sawa naasilimia 3.03 hawakufanya mtihani. 
2.    Watahiniwa wa Shule 
Kwa Watahiniwa wa Shule, kati ya watahiniwa 35,650 waliosajiliwa, watahiniwa 35,418 sawa na asilimia 99.35 walifanya mtihani ambapo wasichana walikuwa ni 11,022 (99.63%) na wavulana ni 24,396 (99.22%). Watahiniwa 232 (0.65%) hawakufanya mtihani. 
3.    Watahiniwa wa Kujitegemea 
Kwa upande wa Watahiniwa wa Kujitegemea, kati ya watahiniwa 6,318 waliosajiliwa, watahiniwa 5,277 sawa na asilimia 83.52 walifanya mtihani na watahiniwa 1,041 sawa na asilimia 16.48 hawakufanya mtihani.

3.    MATOKEO YA MTIHANI 
3.    Watahiniwa Wote 
Jumla ya watahiniwa 38,905 sawa na asilimia 95.98 ya watahiniwa waliofanya Mtihani wa Kidato cha Sita 2014 wamefaulu. Wasichana waliofaulu ni 12,080 sawa na asilimia 97.66wakati wavulana waliofaulu ni 26,825 sawa na asilimia 95.25.

Mwaka 2013 watahiniwa waliofaulu walikuwa ni 44,366 sawa na asilimia 87.85.
3.    Watahiniwa wa Shule
Watahiniwa wa Shule waliofaulu ni 34,645 sawa na asilimia 98.26 ya waliofanya mtihani. Wasichana waliofaulu ni 10,900 sawa na asilimia 99.20 na wavulana ni 23,745 sawa na asilimia97.84.

Mwaka 2013 Watahiniwa 40,242 sawa na asilimia 93.92 ya Watahiniwa wa Shule walifaulu mtihani huo.
3.    Watahiniwa wa Kujitegemea
Idadi ya Watahiniwa wa Kujitegemea waliofaulu mtihani ni 4,260 sawa na asilimia 80.73.Mwaka 2013 Watahiniwa wa Kujitegemea 4,124 sawa na asilimia 53.87 walifaulu mtihani huo.

4.    UBORA WA UFAULU

Ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata Watahiniwa wa Shule unaonesha kuwa jumla ya watahiniwa 30,225 sawa na asilimia 85.73 wamefaulu katika madaraja I – IIIwakiwemo wasichana 9,954 sawa na asilimia 90.59 na wavulana 20,271 sawa na asilimia83.53.

Jedwali lifuatalo linaonesha ufaulu kwa kila Daraja kwa Watahiniwa wa Shule na kwa Jinsi:
Daraja la Ufaulu
Wavulana
Wasichana
Jumla
Idadi
Asilimia
Idadi
Asilimia
Idadi
Asilimia
I
2,232
9.20
1,541
14.02
3,773
10.70
II
6,179
25.46
3,452
31.42
9,631
27.32
III
11,860
48.87
4,961
45.15
16,821
47.71
IV
3,474
14.31
946
8.61
4,420
12.54
0
524
2.16
88
0.80
612
1.74


5.    UFAULU WA MASOMO KWA WATAHINIWA WA SHULE
Jedwali lifutalo linaonesha kuwa ufaulu wa watahiniwa wa shule katika masomo yote (14) ya msingi umepanda ikilinganishwa na mwaka 2013. Ufaulu wa juu kabisa ni ule wa somo laKiswahili ambapo asilimia 99.88 ya watahiniwa wote wa Shule waliofanya somo hilo wamefaulu. Aidha, ufaulu katika masomo ya Sayansi (Physics, Chemistry, Biology na Advanced Mathematics) umeendelea kuimarika kwa kulinganisha na ufaulu wa masomo hayo mwaka 2013.

Na.
MASOMO
WALIOFAULU 2013
WALIOFAULU 2014
IDADI
ASILIMIA
IDADI
ASILIMIA
111
GENERAL STUDIES
16,507
38.53
32,590
92.44
112
HISTORY
18,987
97.33
13,308
99.90
113
GEOGRAPHY
20,578
96.87
19,089
99.48
114
DIVINITY
2,674
90.61
2,280
96.65
115
ISLAMIC KNOWLEDGE
705
57.36
436
73.28
121
KISWAHILI
11,840
96.95
6,384
99.98
122
ENGLISH LANGUAGE
11,081
93.61
8,111
99.04
123
FRENCH
88
91.67
59
98.33
125
ARABIC
801
82.32
443
93.86
131
PHYSICS
5,788
46.34
9,311
78.41
132
CHEMISTRY
13,809
83.87
15,340
95.78
133
BIOLOGY
9,181
87.05
10,693
97.57
134
AGRICULTURE
537
98.35
350
99.72
136
COMPUTER SCIENCE
74
80.43
94
98.95
141
BASIC APPLIED MATHEMATICS
7,827
49.48
11,370
77.39
142
ADVANCED MATHEMATICS
6,895
69.32
8,537
89.40
151
ECONOMICS
8,173
93.53
7,589
99.57
152
COMMERCE
1,573
88.57
821
99.76
153
ACCOUNTANCY
1,660
93.42
819
99.27
155
FOOD AND HUMAN NUTRITION
107
98.17
121
100

6.    SHULE ZILIZOFANYA VIZURI ZAIDI
Ubora wa shule umepangwa kwa kutumia kigezo cha Wastani wa Pointi (Grade Point Average – GPA) ambapo A=1, B+= 2, B=3, C=4, D=5, E=6 na F=7.

Mchanganuo wa upangaji wa Shule zilizofanya vizuri umezingatia shule zenye idadi ya watahiniwa wasiopungua 30.

6.1 Shule kumi (10) bora


Na
JINA LA SHULE
IDADI YA WATAHINIWA
MKOA
1
IGOWOLE S S
30
IRINGA
2
FEZA BOYS’ S S
60
DAR ES SALAAM
3
KISIMIRI S S
52
ARUSHA
4
IWAWA S S
39
NJOMBE
5
KIBAHA S S
167
PWANI
6
MARIAN GIRLS S S
138
PWANI
7
NANGWA S S
97
MANYARA
8
UWATA S S
30
MBEYA
9
KIBONDO S S
62
KIGOMA
10
KAWAWA S S
47
IRINGA

6.2 Shule kumi (10) za Mwisho


Na
JINA LA SHULE
IDADI YA WATAHINIWA
MKOA
1
BEN BELLA S S
105
UNGUJA
2
FIDEL CASTRO S S
69
PEMBA
3
TAMBAZA S S
322
DAR ES SALAAM
4
MUHEZA HIGH SCHOOL
117
TANGA
5
MAZIZINI S S
97
UNGUJA
6
MTWARA TECHNICAL S S
103
MTWARA
7
IYUNGA TECHNICAL S S
158
MBEYA
8
AL-FALAAH MUSLIM S S
37
UNGUJA
9
KALIUA S S
237
TABORA
10
OSWARD MANG’OMBE S S
122
MARA

7.    WATAHINIWA WALIOFANYA VIZURI ZAIDI
Watahiniwa waliofanya vizuri zaidi wamepatikana kwa kuangalia wastani wa Pointi (GPA)kwenye masomo ya tahasusi (combination) pamoja na wastani wa alama za jumla walizopata.

1.    Watahiniwa Kumi (10) Bora kwa Masomo ya Sayansi Kitaifa

Na.
JINA
JINSI
SHULE
MKOA
MCHEPUO
1
ISAACK A SHAYO
M
ST.JOSEPH’S CATHEDRAL
DAR ES SALAAM
PCM
2
DORIS ATIENO NOAH
F
MARIAN GIRLS
PWANI
PCM
3
INNOCENT SABBAS YUSUFU
M
FEZA BOYS’
DAR ES SALAAM
PCB
4
PLACID EZEKIEL PIUS
M
MOSHI
KILIMANJARO
PCM
5
BENNI B SHAYO
M
ILBORU
ARUSHA
PCM
6
ABUBAKAR JUMA
M
MZUMBE
MOROGORO
PCM
7
MWAMINIMUNGU CHRISTOPHER
M
TABORA BOYS
TABORA
PCM
8
CHIGULU JAPHALY
M
MZUMBE
MOROGORO
PCM
9
HUSSEIN PARPIA
M
AL-MUNTAZIR ISLAMIC SEMINARY
DAR ES SALAAM
PCM
10
RAMADHANI ALLY MSANGI
M
FEZA BOYS’
DAR ES SALAAM
PCM

2.    Wasichana Kumi (10) Bora kwa Masomo ya Sayansi Kitaifa:

Na.
JINA
SHULE
MKOA
MCHEPUO
1
DORIS ATIENO NOAH
MARIAN GIRLS
PWANI
PCM
2
MONICA E MTEI
MARIAN GIRLS
PWANI
PCB
3
WEMA KIBANGA
MARIAN GIRLS
PWANI
PCB
4
DEBORAH A MLAWA
MARIAN GIRLS
PWANI
PCM
5
DOREEN P KASHUSHURA
MARIAN GIRLS
PWANI
PCM
6
HEAVENLIGHT M MUNISI
ST.MARY GORETI
KILIMANJARO
PCM
7
FRIDA MBILINYI
MSALATO
DODOMA
PCM
8
AISHA A MNJOVU
FEZA GIRLS’
DAR ES SALAAM
PCM
9
GLORY KWEKA
MSALATO
DODOMA
PCM
10
MULHAT AHMED SAID
FEZA GIRLS’
DAR ES SALAAM
PCM

3.    Wavulana Kumi (10) Bora kwa Masomo ya Sayansi Kitaifa:

Na.
JINA
SHULE
MKOA
MCHEPUO
1
ISAACK A SHAYO
ST.JOSEPH’S CATHEDRAL
DAR ES SALAAM
PCM
2
INNOCENT SABBAS YUSUFU
FEZA BOYS’
DAR ES SALAAM
PCB
3
PLACID EZEKIEL PIUS
MOSHI
KILIMANJARO
PCM
4
BENNI B SHAYO
ILBORU
ARUSHA
PCM
5
ABUBAKAR JUMA
MZUMBE
MOROGORO
PCM
6
MWAMINIMUNGU CHRISTOPHER
TABORA BOYS
TABORA
PCM
7
CHIGULU JAPHALY
MZUMBE
MOROGORO
PCM
8
HUSSEIN PARPIA
AL-MUNTAZIR ISLAMIC SEMINARY
DAR ES SALAAM
PCM
9
RAMADHANI ALLY MSANGI
FEZA BOYS’
DAR ES SALAAM
PCM
10
LUSEKELO A KIHESYA
MPWAPWA
DODOMA
PCM

6.    Watahiniwa Kumi (10) Bora kwa Masomo ya Biashara Kitaifa

Na.
JINA
JINSI
SHULE
MKOA
MCHEPUO
1
JOVINA LEONIDAS
F
NGANZA
MWANZA
ECA
2
NESTORY MAKENDI
M
KIBAHA
PWANI
ECA
3
IMMA ANYANDWILE
M
UMBWE
KILIMANJARO
ECA
4
THERESIA CYPRIAN MARWA
F
LOYOLA
DAR ES SALAAM
ECA
5
GRACE DAVID CHELELE
F
LOYOLA
DAR ES SALAAM
ECA
6
BETRIDA J RUGILA
F
BAOBAB
PWANI
ECA
7
JACQUELINE V KALINGA
F
WERUWERU
KILIMANJARO
ECA
8
TAJIEL ELISHA KITOJO
F
ARUSHA
ARUSHA
ECA
9
SHRIYA SANJIV RAMAIYA
F
SHAABAN ROBERT
DAR ES SALAAM
ECA
10
MWANAID MWAZEMA
F
WERUWERU
KILIMANJARO
ECA

6.    Wasichana kumi (10) Bora kwa Masomo ya Biashara Kitaifa

Na.
JINA
SHULE
MKOA
MCHEPUO
1
JOVINA LEONIDAS
NGANZA
MWANZA
ECA
2
THERESIA CYPRIAN MARWA
LOYOLA
DAR ES SALAAM
ECA
3
GRACE DAVID CHELELE
LOYOLA
DAR ES SALAAM
ECA
4
BETRIDA J RUGILA
BAOBAB
PWANI
ECA
5
JACQUELINE V KALINGA
WERUWERU
KILIMANJARO
ECA
6
TAJIEL ELISHA KITOJO
ARUSHA
ARUSHA
ECA
7
SHRIYA SANJIV RAMAIYA
SHAABAN ROBERT
DAR ES SALAAM
ECA
8
MWANAID MWAZEMA
WERUWERU
KILIMANJARO
ECA
9
VAILETH KALAGO
NGANZA
MWANZA
ECA
10
MARY ROBERT NGOWA
NGANZA
MWANZA
ECA

6.    Wavulana Kumi (10) Bora kwa Masomo ya Biashara Kitaifa

Na.
JINA
SHULE
MKOA
MCHEPUO
1
NESTORY MAKENDI
KIBAHA
PWANI
ECA
2
IMMA ANYANDWILE
UMBWE
KILIMANJARO
ECA
3
KELVIN NZOWA
KIBAHA
PWANI
ECA
4
KIBHULI MWITA
KIBAHA
PWANI
ECA
5
PRINCE MBWATE MWAMBAJA
ST.JOSEPH’S CATHEDRAL
DAR ES SALAAM
ECA
6
ERASTO SONELO
KIBAHA
PWANI
ECA
7
JOEL MATHEW MHANA
KIBAHA
PWANI
ECA
8
SADICK MWANGA LUHEYA
KIBAHA
PWANI
ECA
9
SHEWISHI H RAYMOND
UMBWE
KILIMANJARO
ECA
10
ANTONY VICENT MUSHI
UMBWE
KILIMANJARO
ECA

6.    Watahiniwa Kumi (10) Bora kwa Masomo ya Lugha na Sanaa Kitaifa

Na.
JINA
JINSI
SHULE
MKOA
MCHEPUO
1
LISA VICTOR MIMBI
F
ST.MARY GORETI
KILIMANJARO
EGM
2
ROSALYN A TANDAU
F
MARIAN GIRLS
PWANI
EGM
3
JOSEPH NGOBYA
M
ST.JOSEPH’S CATHEDRAL
DAR ES SALAAM
EGM
4
ANETH D MTENGA
F
MARIAN GIRLS
PWANI
EGM
5
IDDA MICHAEL LAWENJA
F
MARIAN GIRLS
PWANI
HGL
6
EDNA EMMANUEL MWANKENJA
F
KISIMIRI
ARUSHA
HKL
7
CATHERINE J KIIZA
F
ST.MARY’S MAZINDE JUU
TANGA
HKL
8
NANCY ADON SWAI
F
MWIKA
KILIMANJARO
EGM
9
MOHAMED SALMIN
M
MWANZA
MWANZA
HGK
10
IDRISA HAMISI
M
MWEMBETOGWA
IRINGA
HGL

6.    Wasichana Kumi (10) Bora kwa Masomo ya Lugha na Sanaa Kitaifa

Na.
JINA
SHULE
MKOA
MCHEPUO
1
LISA VICTOR MIMBI
ST.MARY GORETI
KILIMANJARO
EGM
2
ROSALYN A TANDAU
MARIAN GIRLS
PWANI
EGM
3
ANETH D MTENGA
MARIAN GIRLS
PWANI
EGM
4
IDDA MICHAEL LAWENJA
MARIAN GIRLS
PWANI
HGL
5
EDNA EMMANUEL MWANKENJA
KISIMIRI
ARUSHA
HKL
6
CATHERINE J KIIZA
ST.MARY’S MAZINDE JUU
TANGA
HKL
7
NANCY ADON SWAI
MWIKA
KILIMANJARO
EGM
8
HADIJA YUSUPH NGONYANI
MWANZA
MWANZA
HKL
9
VICTORIA R NDOSI
ASHIRA
KILIMANJARO
HGE
10
ZUHURA SHABANI MKILALU
MARIAN GIRLS
PWANI
EGM

6.    Wavulana Kumi (10) Bora kwa Masomo ya Lugha na Sanaa Kitaifa

Na.
JINA
SHULE
MKOA
MCHEPUO
1
JOSEPH NGOBYA
ST.JOSEPH’S CATHEDRAL
DAR ES SALAAM
EGM
2
MOHAMED SALMIN
MWANZA
MWANZA
HGK
3
IDRISA HAMISI
MWEMBETOGWA
IRINGA
HGL
4
SELEMAN RAPHAEL NDIKIMINWE
HUMURA
KAGERA
HKL
5
SUNDAY MWAKIPAGALA
ALPHA
DAR ES SALAAM
EGM
6
ERASTO EMMANUEL
KISIMIRI
ARUSHA
HKL
7
MASHAURI FURAHISHA FAUSTINE
MWANZA
MWANZA
HKL
8
EBBY EBAYOTH MALILA
UWATA
MBEYA
HKL
9
CHARLES M ALBERT
PUGU
DAR ES SALAAM
EGM
10
JOSEPH BASILIO
KAWAWA
IRINGA
HGK

8.    MATOKEO YA MTIHANI YALIYOZUILIWA
Baraza la Mitihani la Tanzania limezuia kutoa matokeo ya:
1.    Watahiniwa 150 wa Shule ambao hawajalipa ada ya Mtihani hadi watakapolipa.
2.    Watahiniwa 9 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mtihani kwa baadhi ya masomo. Watahiniwa husika wamepewa fursa ya kufanya mtihani kwa masomo ambayo hawakuyafanya kwa sababu ya ugonjwa katika Mtihani wa Kidato cha Sita Mei, 2015.
3.    Watahiniwa 29 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mtihani kwa masomo yote. Watahiniwa husika wamepewa fursa ya kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita Mei, 2015.

9.    MATOKEO YA MTIHANI YALIYOFUTWA
Baraza la Mitihani la Tanzania limefuta matokeo yote ya watahiniwa wawili (02) waliobainika kufanya udanganyifu katika mtihani.


Baraza la Mitihani la Tanzania linapenda kutumia fursa hii kuzipongeza Kamati za Uendeshaji Mitihani za Mikoa na Wilaya, Wakuu wa Shule na Wasimamizi wa Mtihani uliyofanyika Mei, 2014 kwa kuzingatia na kusimamia taratibu za Uendeshaji Mitihani vizuri na hivyo kuzuia udanganyifu kufanyika. Aidha, Baraza linawapongeza watahiniwa wote waliofanya Mtihani wa Kidato cha Sita, 2014 kwa kutojihusisha na udanganyifu.


10.  KUANGALIA MATOKEO YA MITIHANI
1.    Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) uliofanyika Mei 2014 yanapatikana katika tovuti zifuatazo:
·        www.matokeo.necta.go.tz,
·        www.necta.go.tz au www.moe.go.tz na
·        www.pmoralg.go.tz
2.    Matokeo yanaweza kupatikana pia kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwenda namba 15311. Jinsi ya kutuma ujumbe andika:
MATOKEOXNAMBA_KITUOXNAMBA_MTAHINIWA

(Mfano : matokeoxS0101x0503)

Dkt. Charles E. Msonde
KAIMU KATIBU MTENDAJI

16/07/2014

No comments:

Post a Comment