Uchunguzi wa maradhi ya moyo bure umeanza
jijini Dar es Salaam leo ambako watoto 100 watakaobainika kuwa na maradhi hayo
watapelekwa nchini India kwa matibabu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti
wa hospitali ya Regency ambako uchunguzi huo unafanyika, Dk. Rajni Kanabar
amesema, watoto 100 wenye maradhi ya moyo kutoka Tanzania Bara na Visiwani
watakwenda kutibiwa.
Kambi ya uchunguzi huo imeandaliwa kwa pamoja
baina ya Hospitali ya Regency, Klabu ya Lions ya Dar es Salaam, na Fortis
Escorts Heart Institute ya India India.
Aidha, Dk. Kanabar, amesema kambi hiyo ambayo
imeanza leo itaendeshwa na mtaalamu bingwa wa maradhi ya moyo kutoka Fortis
Escorts Heart Institute ya India, Dk. Ashutosh Marwah.
Dk. Kanabar, amesema uchunguzi huo vile vile
utafanyika Zanzibar kuanzia Agosti 13 na 14 na kuwaomba watanzania wote
kuchangamkia fursa hiyo ili wajue matatizo yanayowakabili watakapokutana na
wataalamu.
Amesema wagonjwa 100 watachaguliwa kwenye kambi
hiyo, kwa ajili ya kwenda kufanyiwa matibabu na upasuaji nchini India, kwa
punguzo kubwa la gharama wakati wengine watafanyiwa bure.
No comments:
Post a Comment