Serikali imewataka viongozi wa dini nchini
kuendelea kuombea taifa libakie na amani, utulivu na upendo miongoni mwa
wananchi, kwani ni tunu kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilalalisema
hayo wakati akizungumza na baadhi ya viongozi wa dini jijini Dar es Salaam.
Dk Bilal amesema viongozi wa dini wanayo nafasi
kubwa ya kufanya waumini wao kutambua umuhimu wa tunu iliyoletwa kwa wanadamu
waweze kukabiliana na majukumu ya maisha yao.
Drt. Bilal amesema amani ndiyo tunu pekee
ambayo Taifa la Tanzania linaendelea kujivunia tofauti na nchi nyingi za Afrika
na ulimwengu kwa ujumla.
Aidha amewasihi viongozi wa dini kusimama
kidete ili kuhakikisha wanailinda amani iliyopo kwa maslahi ya watanzania wote.
No comments:
Post a Comment