Mahujja nchini Tanzania wametakiwa kutumia mafunzo ya Ibada ya Hijja ipaswavyo na kujiepusha na vitendo vyote vinavyoweza kuchafua hadhi yao.
Aidha
wametakiwa kumshukuru sana Mola wao kwa kuweza kukamilisha ibada hiyo adhimu ambayo
pia inakamilisha nguzo ya Tano ya dini tukufu ya Kiislamu.
Wito
huo umetolewa na Samahatu Sheikh Mohammed Ally katika mahojiano maalumu na waandishi
wa habari ofisini kwake micheweni Kisiwani Pemba.
Sheikh
Mohammed amesema, mahujaj ni wageni wa Mwenyezi Mungu, hivyo basi zawadi
walizichuma zinapaswa kutumika katika maisha yao yote ya kila siku.
Amesema,
mahujjaj wanapaswa kuwa ni dira ya jamii wanazotoka hasa kutokana na kasi ya kuporomoka
kwa maadili kunako likabili taifa.
No comments:
Post a Comment