Mtoto mwenye umri wa siku nane, ameibwa baada
ya mama yake kunyweshwa juisi inayosadikiwa kuwa na dawa za kulevya.
Mganga Mfawidhi
wa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma, Dk. Nassoro Mzee, amethibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kusema kuwa mwanamke huyo, Teddy Bishaliza (19), amelazwa katika
Wodi 17 kufuatia afya yake kuathiriwa na dawa hizo.
Akizungumza
wodini hapo, Bishaliza amesema amejifungua mtoto huyo hospitalini hapo kwenye
Wodi Namba Tatu na kuruhusiwa kurejea nyumbani kwake akiwa na mtoto wake.
Amesema akiwa
nyumbani kwake mama yake Bishaliza, amempelekea chakula na akamuacha na mdogo wake, Rahel Leganga (12),
mtoto na mgeni wao huyo.
Amesema, wakati
wakila chakula, mgeni huyo aliyejifungua ushungi aliokuwa amejifunika sehemu
kubwa ya uso wake alimuagiza ampe vikombe ili awawekee juisi ambapo walipomaliza
kula tu alilala.
Rahel amesema
hata yeye baada ya kula alienda kulala na alipoamka saa 11:00 alfajiri, alishangaa
kumkuta dada yake amelala fofofo huku mtoto na mgeni wakiwa hawamo chumbani.
No comments:
Post a Comment