DAR ES SALAAM
Raisi Jakaya Kikwete amesema upo ushahidi
unaothibitisha kuwa baadhi ya mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini wamekuwa
wakichanganya dini na siasa kuunga mkono shughuli za kisiasa za baadhi ya
vyama.
Kufuatia hatua hiyo ambayo Rais ameiita kuwa ni
njia ya hatari, ameomba mabalozi waiokoe nchi katika majanga makubwa yanayoweza
kutokea kutokana na kutumia dini kuendeleza siasa.
Rais ameyasema hayo wakati akizungumza wakati
wa chakula cha usiku na viongozi wa dini nchini wanaoendelea na mkutano wao wa
mwaka jijini Dar es Salaam.
Katika mkutano huo, mabalozi 15
wanaoziwakilisha nchi zao nchini wanahudhuria yakiwamo na mashirika kadhaa ya
kimataifa ikiwa ni pamoja na la Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP).
Mabalozi wanaowakilisha nchi zao katika Mkutano
huo ni wa Ujerumani, Iran, Marekani, Norway, Uturuki, Sweden, Canada, Denmark,
Finland, Misri, Qatar, Uswisi, Palestina, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE),
Saudi Arabia na Umoja wa Ulaya (EU).
No comments:
Post a Comment