DODOMA
Halmashauri ya Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma
imesema haitawavumilia walimu walevi, walimu wa kike wanaovaa mavazi mafupi na
yanayoonesha maungo ya miili yao na walimu wa kiume wanaovaa suruali za kubana.
Kauli hiyo imetolewa na Ofisa Elimu wa Wilaya
ya Bahi, Mary Mathew wakati akizungumza na walimu wapya wa shule za msingi
kwenye semina elekezi inayohusu utendaji wa kazi zao.
Amesema ualimu ni kazi inayohitaji nidhamu ya
hali ya juu kutokana na walimu kuwa walezi wa watoto wanaokuwa wanawafundisha, hiyo
ni vyema wakavaa mavazi ya heshimahasa kutokana na wao kuwa kioo cha jamii.
Amesema ni marufuku kwa walimu kuvaa nguo fupi
na zile zinazoonesha maungo ya miili yao.
Pia amewataka walimu hao kuzingatia miiko ya
kazi kwa mujibu wa waraka na sheria za serikali, ili kuleta ufanisi katika
kuboresha elimu.
Naye, Ofisa Utumishi wa Wilaya ya Bahi Fredrick
Kayombo amewashauri walimu hao kutumia fursa zao katika kuanzisha miradi
itakayowafanya wakopesheke kwenye taasisi za kifedha.
No comments:
Post a Comment