Wednesday, October 8, 2014

KUNDI LA KWANZA LA MAHUJJAJ KUTOKA TANZANIA KUWASILI LEO



DAR ES SALAAM

Kundi la kwanza la mahujja  kutoka Tanzania wanatarajiwa kuwasili hii leo wakitokea katika miji mitukufu ya Makkah na Madina.

Kurejea kwa mahujjaj kutoka miji hio mitukufu kunafuatia kukamilika kwa ibada tukufu ya hijja, ambayo ni nguzo ya tano katika nguzo za dini ya kiislamu.

Wakati kundi hilo la kwanza likitarajiwa kuwasili hii leo nchini Tanzania, baadhi ya mahujjaj wengine wanaendelea na ziara katika mji mtukufu wa madina.

Wakizungumza na Radio Kheri ya jijini Dar es Salaam, baadhi ya viongozi wa mahujjaj wamesema, hadi sasa mahujjaj wote kutoka Tanzania wapo salama.

Hayo yanajiri huku Serikali ya Saudi Arabia ikitangaza kuwa, mahujaji wasiopungua 130 wengi wao kutoka nchi za Kiarabu, wamefariki dunia wakati wa ibada ya Hija mwaka huu.

Hija inahesabiwa kuwa ni moja kati ya nguzo muhimu ya dini tukufu ya Kiislamu, na Waislamu wenye uwezo wa kifedha na kiafya kutoka pembe mbalimbali duniani hushiriki kwenye ibada hiyo katika mji wa Makka.

No comments:

Post a Comment