Sh.
bilioni 840 zinahitajika kutoka kwa wafadhili kila mwaka kwa ajili ya kupambana
na mabadiliko ya tabianchi na kujenga uelewa kwa wakulima juu ya mikakati bora ya
kilimo cha kuhimili ukame.
Mkurugenzi
msaidizi toka Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira, Richard
Muyugi, amesema ipo haja ya kuwaelimisha wakulima ili kuchukua tahadhari mapema
ya mabadiliko ya tabianchi.
Muyungi
ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa kufungua mkutano wa siku mbili
juu ya Mabadiliko ya Hewa na Kilimo.
Amesema
hadi sasa wamepata Sh.bilioni 33.6 kutoka jumuiya ya Ulaya kwa
lengo kusaidia katika mchakato wa utoaji elimu na utekelezaji.
Naye
Afisa kutoka Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Dk.
Kaisa Karttunen, amesema lengo la semina ni kushiriki na kutafuta njia bora ya
kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kilimo chenye kuhimili ukame.
No comments:
Post a Comment