Monday, June 30, 2014

IDADI YA WAISLAMU NCHINI CANADA YAONGEZEKA KWA KASI YA AJABU!




Idadi ya Waislamu nchini Canada imeongezeka na kufikia karibu milioni moja na laki moja. 

Matokeo ya utafiti mpya uliofanywa nchini humo yameonyesha kuwa jamii ya Waislamu huko Canada huwenda ikawa mara tatu zaidi katika kipindi cha miaka 20 ijayo. 

Uislamu ni dini ya pili kwa ukubwa huko Canada baada ya dini ya Kikristo na ni ya kwanza katika dini zinazoenea kwa kasi nchini humo. 

Kituo cha sensa ya watu nchini Canada kimetangaza kuwa, ni Waislamu 13 pekee wa Ulaya ndio walikuwepo huko Canada wakitokea Bosnia-Herzegovina, miaka minne baada ya kuundwa nchi hiyo mwaka 1867. 

Licha ya vyombo vya habari vya Magharibi kuendesha propaganda kubwa za kueneza chuki na hofu dhidi ya Uislamu, lakini hali hiyo imeshindwa kuzuia mvuto wa dini hiyo nchini humo.

Aidha, licha ya kuwepo vitendo vya kufurutu mpaka vinavyofanywa na watu wasio na uelewa sahihi wa Uislamu na hivyo kuathiri mtazamo wa walimwengu juu ya dini hiyo, lakini yote hayo hayajaweza kupunguza mvuto na ongezeko la watu wanaoamua kuingia katika dini Tukufu ya Uislamu

Hii imekuja kutokana na takwimu kuonyesha kuwa Uislamu ndiyo dini inayokua kwa kasi zaidi katika nchi za Magharibi.






No comments:

Post a Comment