Monday, June 30, 2014

MTANDAO WA FACE BOOK LAWAMANI, WATUMIAJI TAHADHARINI:



 
Mtandao wa Facebook umelaumiwa kwa kuwafanyia wateja wake utafiti wa kisaikolojia bila ya kuwajulisha.

Nia ya utafiti huo ilikuwa ni kujua kama wateja wake wamebadili tabia ya kuweka picha na mawazo yao katika mtandao huo kutokana na kukasirishwa na tabia za baadhi ya watumiaji wenzao.

Aidha, utafiti huo umeohusisha takribani watumiaji 700,000 na unaonyesha kuwa Facebook inacheza na taarifa za watumiaji wake ili kupata hisia zao katika kile wanachokiweka kwenye mtandao huo.

Hata hivyo mtandao wa Facebook umekanusha madai hayo na kwamba hakuna mtumiaji binafsi aliyelengwa na utafiti huo uliofanywa na mtandao huo kwa ushirikiano na chuo kikuu cha Cornell na California.

Waziri wa kazi Jim Sheridan mjumbe wa bodi ya mawasiliano ameagiza uchunguzi kufanyikadhidi ya mtandao huo wa Facebook katika tuhuma hizi.

Hata hivyo Katherine Sledge Moore, Profesa wa Saikolojia katika chuo cha Elmhurst , Illinois amesema kwa jinsi ambavyo Facebook wamekuwa wakishughulika na taarifa za wateja wake makubaliano yaliyopo katika utafiti huo hadhani kama yapo nje ya hali ya kawaida.


Adam Kramer kutoka Facebook mmoja kati ya walioandaa taarifa ya utafiti huo amesema wanadhani kuwa ilikuwa mhimu kwao kutafiti mashaka yanayowakumba watumiaji hasa katika mawazo yanayowekwa na marafiki zao na jinsi yanavyowafanya wafikirie tofauti .






No comments:

Post a Comment