Friday, October 17, 2014

KICHANGA CHAIBWA!



Mtoto mwenye umri wa siku nane, ameibwa baada ya mama yake kunyweshwa juisi inayosadikiwa kuwa na dawa za kulevya.


Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma, Dk. Nassoro Mzee, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mwanamke huyo, Teddy Bishaliza (19), amelazwa katika Wodi 17 kufuatia afya yake kuathiriwa na dawa hizo.


Akizungumza wodini hapo, Bishaliza amesema amejifungua mtoto huyo hospitalini hapo kwenye Wodi Namba Tatu na kuruhusiwa kurejea nyumbani kwake akiwa na mtoto wake.


Amesema akiwa nyumbani kwake mama yake Bishaliza, amempelekea chakula na  akamuacha na mdogo wake, Rahel Leganga (12), mtoto na mgeni wao huyo.


Amesema, wakati wakila chakula, mgeni huyo aliyejifungua ushungi aliokuwa amejifunika sehemu kubwa ya uso wake alimuagiza  ampe vikombe ili awawekee juisi ambapo walipomaliza kula tu alilala.


Rahel amesema hata yeye baada ya kula alienda kulala na alipoamka saa 11:00 alfajiri, alishangaa kumkuta dada yake amelala fofofo huku mtoto na mgeni wakiwa hawamo chumbani.




No comments:

Post a Comment