Ibun jazar Islamic schools
NA INSHAALLAH IPO SIKU ITATIMIA.
Moja
ya ndoto zangu ni siku moja kuiona Ibun Jazar ni shule moja miongoni mwa shule zinazofanikiwa na kusifika kwa
matumizi ya Lugha ya Kiingereza na Kiarabu kama lugha za mawasiliano miongoni mwa wanafunzi, walimu na kwa
watumishi wengine pia.
Huenda
wakawepo wenyemawazo ya kuwa suala hilo haliwezekani, na wakajaribu kujenga hoja nyingi tu kuthibitisha madai yao. Ima
kutokana na jitihada ambazo zimejaribiwa kuchukuliwa hapo awali na hatimaye
kuonekana kushindwa kufanikisha suala hilo.
Napenda ieleweke kwamba kukosea kupo na sisi huenda tulikosea mapema kwa kutokuzingatia uteuzi
wa watumishi kulingana na mahitaji
ya Jazar yenyewe.
Aidha
tumeshindwa
kuieleza falsafa na mwelekeo wa Jazar kwa
watumishi wetu jambo ambalo limefanya suala la kuzungumza Kiswahili ni jambo la
kawaida na kamwe haliwezi kubadilika. Lakini alhamdu lillah, Jazar inabarka ya watumishi wake wengi wenye uwezo wa kuzungumza
kiingereza au kiarabu na kizuri zaidi kunakitengo cha Qur`an ambacho masomo
yake hufundishwa kwa kiarabu.
Vile vile uwajibikaji umekua ni tatizo kubwa, sio kwa Jazar tu bali kwa taasisi nyingi
za kiislamu, unaosababishwa na mazoea katika kazi, baadhi ya watumishi kutokubali
mapungufu yao, huku wakiamini kuwa siku zote wao ndio wanaopatia na wengine ni
watu wa kukosea tu, kutokuaminiana katika mgawanyo wa majukumu, majungu kazini,
kudhaniana vibaya na kutokufanya kazi kwa umoja.
Jitihada
zetu za kupambana katika kutibu ugonjwa huu zimekua zikifeli kutokana na
kujaribu kitibu ugonjwa usiofanyiwa vipimo, huenda daktari akakupa vidonge vya malaria lakini kumbe ulipoenda
kupima katika zahanati nyingine ukagundulika ni maradhi yasiyohitaji vidonge
hivyo.
Mara
zote tumekuwa wakali sana kuwalazimisha watoto kuzungumza kiingereza au kiarabu
wanapokuepo madarasani, lakini watoto haohao husikika wakizungumza Kiswahili katika
halaqaat
za qur`an, wanapokuwepo katika dahalia
zao, wanapotumwa na walimu wao, wakati
wa mapumziko au michezo, na huzungumza
na walimu zao au watumishi wengine wasiokuwa walimu.
Kwa hakika
hajulikani mwalimu wa kiingereza ni yupi, wa kiarabu ni yupi, mwalimu wa Qur`ani
ni yupi, matron na hata patron. Wote wanazungumza Kiswahili. Kwa hali kama hii gonjwa kwetu limekomaa
kuliko kwa hawa watoto, hebu basi tutumbueni la kwetu haraka huku tukikamua
kamua kwa watoto.
Kwa hakika
haya ni maandalizi mabovu ambayo yanapaswa kukemewa na kila mtumishi ikiwa
tunania ya kutengeneza na tuna malengo tuliyoyakusudia.
Kunahoja
zinaweza zikajengwa kuwa mbona kuna baadhi ya shule sizo za bweni lakini
ukifika watoto wanazungumza kiingereza na sio Kiswahili? Ni swali zuri sana ila
kwa msomi wa lugha anafahamu (How community play the great role on
language learning), lakini hata
hao waliofanikiwa kwa njia kama hiyo ni baada ya kutengeneza mazingira ya ndani
ya shule kuanzia kwa mlinzi, matroni, patroni, sekretari na walimu.
Lakini
kama haya ni baadhi ya mapungufu, jee ndio tuseme tumeshindwa? Jee hakuna njia
mbadala za kufanikisha hili? Jibu zipo njia mbadala nyingi tu za kufanikisha
hilo.
Kwanza, umoja na mshikamano. Kutokana na muundo wa kituo cha Ibun Jazar kilivyo na miundo mbinu yetu ni lazima viongozi
(walimu wakuu) kushirikiana na walimu wa lugha,
walimu wa taaluma, walimu wa nidhamu, wakuu wa idaya ya lugha, matron na patron
bila kujali upremari au usekondari, katika kulitekeleza hili.
Pili, Ipo haja suala hili
liwekwe kama moja kati ya kosa la uvunjifu wa nidhamu kwa mtumishi na mwanafunzi atakaebainika akitumia lugha isiyokua
kiingereza au kiarabu kwa maksudi. Iwe darasani, nje ya darasa,
bwenini, na hata kipindi cha michezo
maadamu bado yupo ndani ya eneo la shule.
Tatu, kuanzishwe masomo ya
ziada ya lugha kwa watumishi na
baadhi ya wanafunzi walio na matatizo au mapungufu katika matumizi ya lugha
hizo.
Ninaimani
nitakua nimeeleweka kwa kiasi kikubwa. Haya ni mawazo yangu ninaweza nikapatia
na pia kukosea. Kwa pale nilipopatia nauomba uongozi kwa upande wa Msingi na
Sekondari kuyachukua mawazo haya na kuyafanyia kazi haraka iwezekanavyo. Na kwa
pale nilipokosea, naruhusu kukosolewa na nakaribisha maoni mengine kwa nia ya
kujenga na kuiendeleza Jazari na kuusaidida uislamu.
Aidha,
Jambo hili litasaidia kupunguza mazaungumzo yasiyonaumuhimu (porojo) kwa wanafunzi
na watumishi na kujikita katika kufanya kazi.
Mwisho
nawaomba tufanyekazi kwa pamoja, upendo na mshikamano ili kufanikisha malengo
yetu tuliyoyakusudia tukiamini kuwa Allah ndiye mlipaji.
Mkuu
wa Idara ya lugha Sekondari
Mujbaraka Ghulaam ______________
No comments:
Post a Comment