Wednesday, July 30, 2014

JEE TUMETUBIA TOBA YA KWELI?



RAMADHANI NI MWEZI WA TOBA, JEE TUMETUBIA TOBA YA KWELI? 

WASWAHILI HUSEMA “KUTANGULIA SI KUFIKA”

             Sifa njema zinamstahiki Allah (SW) ambaye amenichagua mimi na wewe msomaji wa makala hii kuzaliwa ilhali tukiwa na shahada kamili ya kukubalika kuwa waislamu, na rehma na amani zimshukie mtukufu wa darja Mtume (SAW) ambaye ameletwa kuwa mkombozi wa haki, usawa na uadilifu.

               Awali ya yote, tumshukuru Allah (SW) kutujaalia kuweza kuudiriki mwezi mtukufu wa ramadhani hadi kufikia kuukamilisha kwake. Tumuombe Allah (SW) atutaqabalie swaumu zetu, visimamo vyetu,  na ibada zetu kwa ujumla.

Allah (SW) ametuletea mwezi mtukufu wa ramadhani, ambao umesifika kwa sifa kumtu, kama vile; ramadhani kuwa ni mwezi wa rehma, mwezi wa maghfra (toba) au msamaha, na nimwezi ambao waja wa Allah (SW) huachwa huru na moto.

Ni jambo la kawaida kwa mswahili kusikika akisema “kutangulia si kufika” vivyo hivyo, nachelea kusema kuwa tumefika safari yetu lakini huenda ikawa tumekwama sehemu fulani au tumetangulia bila kufika safari yetu.

 Tunapozungumzia “toba” tunamaanisha kukusudia  kurejea kwa Mola mlezi kwa kujiepusha na  madhambi au maasi ya aina zote huku mja akijutia  kwa yale aliyoyafanya na kuazimia kutokurudia tena katika madhambi au maasi hayo na akitaraji msamaha wa Allah (SW).

Kimsingi hii ndio maana ya tauba(toba), ambayo ingembidi kila muislamu aipupie na kudumu nayo katika maisha yake ya kila siku akitambua kuwa, suala la tauba (mja kurejea kwa mola wake) ni suala la lazima.

Kurejea kwa Allah (SW) ni jambo la lazima na lililogogotezwa katika kitabu kitukufu cha Quran na Sunna ya Mtume Muhammad (SAW), kama Quran inavyothibitisha katika (sura ya 66:8), pale Mola mlezi anaposema:
“ Enyi mlio amini! tubuni kwa Mwenyezi Mungu toba iliyo ya kweli! asaa Mola wenu Mlezi akakufutieni maovu yenu na akakuingizeni katika pepo zipitazo mito kati yake, siku ambayo Mwenyezi Mungu hatamdhalilisha Nabii na walio amini pamoja naye. Nuru yao inakwenda mbele yao na pande zao za kulia, na huku wanasema: Mola wetu Mlezi! tutimilizie nuru yetu, na utughufirie! hakika Wewe ni mwenye uweza juu ya kila kitu. (Surat Attah'riim, 66:8)

Pia Allah mlezi amesema:
“…Na tubuni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi waumini, ili mpate kufanikiwa. (Suratun nur, 24:31)
            Aidha, imegogotezwa na Mtukufu wa darja, Bwana Mtume (SAW), pale aliposema:
“Mwenye kutubia ni kipenzi cha Allah (S W)             
Tukiangalia maana ya toba kama ilivyofafanuliwa hapo juu, huenda tukarejea katika msemo uleule wa waswahili usemao, kutangulia si kufika.

Hii ni kutokana na kuwa msingi wa kimaana wa tauba umebeba mihimili imara inayoshikilia maana hiyo, jambo linalojidhihirisha kuwa masharti ya kukubalika kwa tauba hiyo.

Masharti hayo ni pamoja na kujuta kwa sababu ya kufanya dhambi, Kuacha kwa haraka dhambi yenyewe, kuazimia kutokurejea tena dhambi hiyo baada ya kutubia na ikiwa dhambi ni katika haki ya mja, inabidi kwanza irudishwe haki hio kwa mwenyewe au umuombe msamaha kwanza ndio utakubaliwa toba yako na Allah (S.W)

Hapa ndipo ninapata wasiwasi juu ya safari yetu hii ya kukamilika kwa mwezi mtukufu wa ramadhani ambayo tayari tumetia nanga. Sijui kama kweli tumefikia kwenye toba hii ya kweli aliyoilingania Allah Mlezi.
  
Katika hili, nimeona kuwa tumeweza kugawanyika katika makundi takriban matatu. Kundi la kwanza ni kundi la waja waliotubia tauba ya kweli, ambalo kiukweli kundi hili ni wachache katika wengi tulioingia katika ibada hii tukufu ya Allah (SW).

Pia, wapo waliotubia ndani ya mwezi wa ramadhani, lakini wakarejea katika maaswi baada tu ya kuindama mwezi huu wa Shawwal, kisha wakajuta na kuzilaumu nafsi zao na kutamani kutokurejea tena katika maaswi hayo.

Aidha, wapo wale waliomlilia Allah (SW) ndani ya mwezi mtukufu wa ramadhani ukweli wa kumlilia, lakini wamezibatwilisha toba zao ndani ya usiku mmoja tu wa Eidilfitri, na kurejea katika maaswi yao kama walivyokuwa kabla ya mwezi wa ramadhani. Hawa wamekula hasara duniani na akhera, wala haikuwa na tija biashara yao hiyo.

      Ndugu yangu msomaji wa makala hii, kiuhakika kila mmoja ni mjuzi juu ya nafsi yake, hebu nisaidie jibu la swali hili, Jee tumefika safari yetu au kutangulia si kufika? Jibu unalokichwani mwako.
Ninamuomba Mola Mlezi atutaqabalie tauba zetu, azithibitishe imani zetu, na atujaalie katika wale waliotubia tauba ya kweli. Ya Allah ! badilisha maovu yetu kuwa mema, zifanye nafsi zetu kuwa ni nafsu l mutwmainna zitakazonadiwa siku ya hukumu na mola zikiambiwa rejeeni kwa Mola mlezi hali ya kuwa mumeridhika na kuridhiwa.

Makala hii imetayarishwa na Muhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kitivo cha lugha za kigeni na sayansi ya lugha.
Mubaraka   Ghulaam.
                                                                                    Sim no. 0777663795 au0717169464
SIKILIZA RADIO KHERI 104.1FM
“ NI FARAJA KWA UMMA FARAJA KWA WAISLAMU!”
                                  

Tuesday, July 29, 2014

SUMATRA IWAJIBISHWE




Chama cha Kutetea Abiria Tanzania (Chakua), kimemuomba Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, kuwawajibisha watendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafirishaji Nchi Kavu na Majini (Sumatra), kutokana na kushindwa kuwatetea abiria.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chakua, Hassani Mchanjama, amesema tangu kuanzishwa kwake, Sumatra imeshindwa kusimamia sheria na kanuni za usafirishaji, kufanya abiria waibiwe na watoa huduma hizo za usafiri.

Mchanjama amesema wamefikia hatua hiyo baada ya kubaini mamlaka hivyo imeshindwa kusimamia huduma za usafiri wa abiria, kitendo kinachowafanya watoaji wa huduma kuamua kutoza nauli wanazotaka kinyume na bei elekezi ya serikali.

Amesema ushahidi wa abiria kupandishiwa nauli holela upo na kila mara wanapopata malalamiko kutoka kwa abiria, wamekuwa wakiiandikia Sumatra barua kuijulisha wizi unaofanyika.


WANAWAKE WAASWA KUTOA SADAKA SIKU YA IDDI



 

Wanawake wa kiislamu wametakiwa kiutumia siku kuu hii ya Eidil fitri katika kuwaangalia wagonjwa, mayatima, wajane na wale wasiojiweza kwa kuwapatia sadaqa ili kuzidi kuzitakasa swaumu zao.

Wito huo umetolewa na Imamu msaidizi wa masjid Msufini jijini Dar es Salaam, Samahatu sheikh Amour Iddi wakati wa khotuba ya swala ya Iddil fitri iliyoswaliwa msikitini hapo mapema hii leo.

Sheikh Amour amesema, wanawake hawanabudi kuzitakasa saumu zao kwa sadaka kutokana na wingi wa kutamka maneno yasiyomazuri bila hata ya kukusudia.

Aidha ametumia fursa hiyo kuwataka waumini hao kuzihifadhi nafsi zao katika kuelekea kumuaswi Mola wao mlezi ndani ya siku hii tukufu ya Iddil fitri, kwani kufanya hivyo kutabatilisha matendo yao ikiwemo ibada tukufu ya Swaumu.

Kwa upande wake, Imam Mkuu wa masjid Msufini, sheikh Qassim Iddi amewataka waislamu kufurahia siku ya Iddi kwa kutembelea maeneo matukufu yakiwemo makaburi ili kupata mazingatio ya siku ya hisabu, jambo ambalo litazidisha uchamungu na kupambana na nafsi zao.



Sunday, July 27, 2014

JEE MWEZI UMEENDAMA AU UMEENDAMISHWA? NANI KAUONA? NA WAPI?



HIVI NDIO MAMBO YALIVYO KUHUSU  MWANDAMO WA MWEZI WA SHAWWAL (1435) &EID IL FITRI JUMAPILI 27TH JULY 2014
 AKILI KICHWANI MWAKO!
Kwahisani ya:

BY MUBA
Taarifa za mwandamo wa mwezi wa Shawwal (Eid il fitri) 1435 zilianza kusubiriwa kwa hamu tokea siku ya jumamosi ya tarehe 26th July 2014, kutokana na baadhi ya nchi kuwa zilikwisha weka matumaini ya kuonekana kwa mwezi mwandamo. Hata hivyo kwa mujibu wa wataalamu wa elimu ya mienendo ya mwenzi hakuna nchi yeyote iliyofanikiwa kuuna mwezi mwandamo kutokana na kutokuwepo uwezekano wa kuonekana kwake.
Nigeria:
    1. Haukuonekana: Kareem Isa (mjumbe wa MCW) kutoka  Abuja Kado alikua na haya ya kusema, “leo ni Ramadhani 29 hapa na ni sawa na tarehe 26th July 2014. Kwa kiasi kuna mawingu mawingu, na nimejaribu kufuatilia tokea 19:00 hadi 19:20  na hakuna taarifa za mwezi kuonekana.   
SUNDAY, 27 JULY 2014:
Mwezi hautarajiwi kuonekana takribani ulimwengu mzima, ispokuwa unaweza kuonekana kwa taabu katika bara la Amerika Kusini, na unaweza kuonekana kwa uwazi katika visiwa vya Polysenia, ambapo huko kuna maripota wetu wa kiislamu wachache.  Na kuna uwezekano mdogo mno kwa nchi ya Afrika Kusini hata hivyo ni wale tu wenyeuzoefu wa uchunguzaji wa mwezi mwandamo ndio wengeweza kuuona mwezi.  
  • Australia:
    1. Haukuonekana: Shahidi ni mwakilishi wetu Abbas Aly (MCW) kutoka  Annangrove NSW amesema: 27th July 2014, kulikua na mawingu madogomadogo, hivyo mwezi haukuweza kuonekana kwa macho matupu. Wanakamilisha ramadhani 30, Eid Jumanne.
   
 
    1. Mwakilishi mwengine ni  Engr Manzoor A Mian (MCW mwanahabari wetu) akiwepo Melbourne, VIC akiripoti kuwa Eid ni Jumanne, July 29th .
    2. Mwengine ni Dr. Shabbir Ahmed (MCW mwanahabari wetu) Imam wa masjid Rooty Hill Mosque Sydney, NSW  
  • Brunei:
    1. Haukuonekana: Na mwanahabari wetu, Dr. Mohammed Hussain Ahmad, amesema mwezi haukuonekana na umetangazwa kupitia televisheni ya taifa kuwa watakamilisha siku 30 za Ramadhani. Hivyo Eid kuwa Jumanne 29th July 2014-
  • China:
    1. Haukuonekana: mwanahabari wetu Dr. Musa·Minhai (MCW member) akiwepo Linxia Gansu Province amesema mwezi haukuonekana ingawa baadhi ya MAULAMAA wametoa fatwa ya kuwa kesho ni Eid, na kufanya waumini kugawika na wengine kusherehekea Eid Jumanne 29th July 2014 wakikamilisha siku 30
    2. Chile. umeonekana/ taarifa kamili tutawaletea zitakapothibitika.
  • Fiji Islands:
    1. Haukuonekana:   Eid ni jumanne 29th July 2014.   
  • Ghana:
    1. Haukuonekana:  
  • India: haukuonekana. Hali ya anga iligubigwa na mawingu.
  • Indonesia:
    1. Haukuonekana: Anga ilikuwa nzuri licha ya kuwepo kwa mawingumawingu. Hata hivyo waziri wa masuala ya kidini kwa kutumia njia ya makadirio ya mahesabu, ameweza kutangaza siku ya kwanza ya shawwal kuwa ni Jumatatu ya tarehe 28th July 2014, hivyo kesho kuwa Eidil fitri .    
  • Kenya:
    1. Haukuonekana: Na mwanahabari wetu: Ali Mohamed kutoka  Mombasa   
       Hali ya anga ilikuwa safi  hata hivyo mwezi haukuonekana

  • Morocco:
    1. Haukuonekana: Eid ni Jumanne 29th July 2014.
  • New Zealand:
    1. Haukuonekana: Eid ni Jumanne    29 July 2014.
  • Oman:
    1. haukuonekana: Na mwanahabari wetu Habibur Rahman Farooqui akiwa Oman   Eid itasherehekewa jumanne 29.07.2014 imetangazwa na kamati ya ufuatiliaji wa mwezi mwandamo.
  • Qatar:
    1. Wametangaza: Na mwanahabari wetu: Muhammad Imran Paracha akiwepo Doha amesema: Wizara ya Fatwa na masuala ya kidini imetangaza kuwa jumatatu 28th July 2014 ni siku ya Eid bila kueleza mwezi umeonekana wapi, hivyo kuonesha kuwa wamefuata Saudi.  
  • Saudi Arabia:
    1. Haukuonekana: Na mwanahabari wetu Sheik A.A. Ishola akiwepo Makkah amesema:  licha ya kufatiliwa kwa umakini mwandamo wa mwezi, lakini umeshindikana kuonekana kutokana na hali ya anga kufunikwa na mawingu.    
    2. Mwezi umetangazwa:  Na mwanahabari wetu, Najeeb Qasmi akiwepo Saudi Arabia amesema: hapa Saudia Eid itafurahiwa kesho, Jumatatu 28th July 2014 kama mahakama ya Saudia ilivyokwisha tangaza kwamba mwezi muandamo umeonekana, licha ya kutokueleza umeonekana wapi, na umeshuhudiwa na nani.
  • South Africa:
    1. Haukuonekana: Na mwandishi wetu, Dr. Husain Sayanvala akiwepo Johannesburg    
    2. Umeonekana: Na mwandishi wetu, Mahmood (Bhaai) Cassim akiwepo   Johannesburg amesema radio ya Kiislamu, ML Bham imetangaza kuwa Eid itakuwa kesho Jumatatu, (28 July) mwezi umeonekana katika maeneo ya mabonde ya kaskazini, na Lenasia kusini.
TAARIFA HII IMELETA UTATA: Kutokana na kupatikana kwa taarifa hii, imetulazimu kuwasiliana na wanahabari wetu wengine wengi na wamesema hali ya mawingu ilikua ni nzuri, na kiukweli hakuna taarifa za ukweli juu ya kauli hii.
    1. Umeonekana: Na mwanahabari wetu Moustafa Sanouss amesema, Nimeweza kuongea na Jopo la Maulamaa kutoka South Africa Johannesburg na wamenithibitishia kuwa mwezi umeonekana katika maeneo tofautitofauti, nah ii hiki hapa ni nchanzo ambazo unaweza kuwasiliana nao   http://www.jmtsa.co.za/contact-us/head-office/
Kauli hii pia imedadavuliwa na Moonsighting.com: Tumejaribu kuwasiliana na wanahabari wetu wote walioko South Africa, na wengi wao wamesema mawingu yalikuwa mazuri na hakuna kamati yeyote ya mwandamo wa mwezi ambayo imeweza kuona mwezi mwandamo. Hivyo suala la kuonekana kwa mwezi muandamo Afrika kusini ni Utata.  
    1.  
  • Tanzania:
    1. Haukuonekana: Mwanahabari wetu Hamza Rijal akitokea visiwani    Zanzibar     
       
  • Yemen:
    1. Wamekamilisha siku 30: Na mwanahabari wetu khadija Mohamed akitokea Yemen reported: wayemeni wamekamilisha siku 30 hivyo Eid itakuwa Jumatatu.

SIKU RASMI YA KWANZA YA SHAWWALI KATIKA NCHI MBALIMBALI NI KAMA IFUATAVYO

JUMAPILI, 27 July 2014:
  1. Hijri Committee of India, kikundi kidogo cha wahindi  
  2. Nigeria (waliotangaza mwezi kimakosa kutokana na lawama za mwandamo wa mwezi )  

JUMATATU, 28 JULY 2014:
  1. Afghanistan (wamewafuata Saudia )
  2. Albania (wamewafuata Saudia
  3. Algeria (wamewafuata Saudia)
  4. Armenia (wamewafuata Saudia)
  5. Austria (wamewafuata Saudia)
  6. Azerbaijan (wamewafuata Saudia)
  7. Bahrain (wamewafuata Saudia)
  8. Bangladesh (baadhi ya maeneo wamewafuata Saudia)
  9. Belgium (wamewafuata Saudia)
  10. Bolivia (wamewafuata Saudia)
  11. Bosnia and Hercegovina (wamewafuata Saudia)
  12. Bulgaria (wamewafuata Saudia)
  13. Canada (kutokana na baraza la fatwa la N/Amerika)
  14. Chechnia (wamewafuata Saudia)
  15. China (Waliowengi wamefuata kalenda ya Makka MeccaCalendar.org)
  16. Cosovo (wamefuata Turkey)
  17. Croatia (wamefuata Turkey)
  18. Denmark (wamewafuata Saudia)
  19. Egypt – mwezi ulizaliwa kabla ya jua kuzama & moon ulibakia kwa muda wa dakika 5 baada ya jua kuzama.   
  20. Fiji Islands http://www.fianz.co.nz/eid-ul-fitr-1435h
  21. Finland (wamewafuata Saudia)
  22. France (umoja wa waislamu wa Ufaransa)  
  23. Georgia (wamewafuata Saudia)
  24. Hungary (wamewafuata Saudia)
  25. Iceland (wamewafuata Saudia)
  26. Indonesia (Inadaiwa kuona – wametangaza rasmi)
  27. Iraq (wamewafuata Saudia)
  28. Ireland (ECFR - European Council for Fatwa and Research)
  29. Italy (Follow Saudi)
  30. Jordan (Follow Saudi)
  31. Kazakhstan (Follow Saudi)
  32. Kenya (Claims of sighting)
  33. Kuwait (Follow Saudi)
  34. Kyrgizstan (Follow Saudi)
  35. Lebanon (Follow Saudi)
  36. Luxembourg (ECFR - European Council for Fatwa and Research)
  37. Macedonia (Follow Turkey)
  38. Malaysia (Age > 8 hours, altitude > 2°, elongation > 3°)
  39. Mauritania (Follow Saudi)
  40. Montenegro (Follow Turkey)
  41. Netherlands (Follow Saudi)
  42. New Zealand (Federation of Islamic Association of New Zealand) http://www.fianz.co.nz/eid-ul-fitr-1435h
  43. Norway (Some follow Saudi)
  44. Palestine (Follow Saudi)
  45. Philippines (Follow Saudi)
  46. Qatar (Follow Saudi)
  47. Romania (Follow Saudi)
  48. Russia (Follow Turkey)
  49. Saudi Arabia (Official Announcement)
  50. Serbia (Follow Turkey)
  51. Slovania (Follow Turkey)
  52. South Africa (Local Sighting)
  53. Spain (Some Follow Saudi)
  54. Sudan (Follow Saudi)
  55. Sweden (Follow Saudi)
  56. Switzerland (Follow Saudi)
  57. Syria (Follow Saudi)
  58. Taiwan (Follow Saudi)
  59. Tajikistan (Follow Saudi)
  60. Tatarstan (Follow Saudi)
  61. Tunisia (Criteria of age, or altitude, or sunset-moonset lag)
  62. Turkey (Somewhere on the globe Altitude > 5°, elongation > 8°)
  63. Turkmenistan (Follow Saudi)
  64. U.A.E. (Follow Saudi)
  65. UK (Follow Saudi) [Coordination Committee of Major Islamic Centres and Mosques of London]
  66. UK (Local Sighting) [Wifaaqul ulama), (Ahle Sunnat Wal Jamaat], OR (Sighting from South Africa)
  67. USA (FCNA/ISNA - Fiqh Council of North America/Islamic Society of North America)
  68. Uzbekistan (Follow Saudi)
  69. Yemen (Completed 30 days)
  70. Zimbabwe (South Africa Sighting)

TUESDAY, 29 JULY 2014:
  1. Australia (watauona kwa jocho la wazi)
  2. Brunei (watauona kwa jocho la wazi)
  3. China (Some follow Local Sighting)
  4. India (Local Sighting)
  5. Iran (Local Sighting)
  6. Morocco (Local Sighting)
  7. Oman (Local Sighting)
  8. Spain (Some Follow Morocco)
  9. Sri Lanka (Local Sighting)
  10. Tanzania (Local Sighting)