Wednesday, August 13, 2014

VIONGOZI WENGINE WA UAMSHO MBARONI ZANZIBAR! YUMO AMIR MSELEMU ALLY




Amir wa Jumuiya ya UAMSHO sheikh Msellem bin Ali na Katibu wake Sheikh Abdallah Madawa wanadaiwa kukamatwa wakiwa wanatoka mahakamani kusikiliza kesi yao.
  



Habari kamili tutakuletea baadae! uchunguzi kwanza unaendelea.

Tuesday, August 12, 2014

WATANZANIA WAISHIO NJE YA NCHI WALIA NA URAIA PACHA



Watanzania  wanaoishi Nchi za Nje wamekodi mtaalamu mbobezi wa masuala ya uraia na kuomba ruhusa kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalumu, Samuel Sitta, ili atoe ufafanuzi kuhusu sura ya tano ya rasimu ya pili ya katiba inayozungumzia masuala ya uraia, ikiwamo uraia pacha.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuwapo lwa mtaalamu huyo, ambaye ni Profesa Boneventure Rutinwa, kwenye baadhi ya kamati, Katibu wa Bunge Maalum, Yahaya Khamis  Hamad, amesema wananchi hao wamemwandikia maombi hayo Bwana Sitta.

Hata hivyo, Profesa Rutinwa ameeleleza kuwa, kazi hiyo ilitakiwa kufanyika Alhamisi na Ijumaa, wiki iliyopita lakini kutokana na Ijumaa kuwa sikukuu ya Nane Nane, alilazimika kuiahirisha

Kwa mujibu wa Profesa Rutinwa, ametakiwa kutoa ufafanuzi kwenye eneo hilo ndani ya kamati zote 12, kwa muda wa saa Moja lakini ameweza kuhudumia kamati tatu tu, kutokana na kuwepo uhitaji mkubwa wa ufafanuzi.

DRT. SHEIN: ZANZIBAR NI AMANI KARIBUNI KWA UTALII!




Raisi wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi, Alhajj Drt. Aliy mohammed Shein, ameitaka Ujerumani kuekeza visiwani humo na kuleta watalii wengi kufuatia kuimarika kwa amani visiwani humo.

Dkt. Shein ameyasema hayo wakati alopokutana na Balozi mpya wa Ujerumani nchini, Ego Kochanke Ikulu mjini Zanzibar

Amesema uhusiano wa Zanzibar na Ujerumani ulianza muda mrefu tangu karne ya 19, ambayo nchi hiyo ilikua miongoni mwa mataifa machache yaliyoyatambua Mapinduzi ya Zanzibar.

Aidha Dkt. Shein ameitaka Ujerumani kuleta watalii wengi visiwani humo kwani sekta hiyo imeweza kuimarika sana kutokana na amani na utulivu wa visiwa hivyo.

Kwa upande wake balozi wa Ujerumani, Ego Kochanke ameipongeza Tanzania kwa kudumisha amani na utulivu na kuahidi kuzidi kuimarisha uhusiano mzuri kati ya nchi hizo.


BAMITA LAITAKA BUNGE MAALUMU LA KATIBA KUJITATHMINI KWANZA!




Baraza la Maadili la Kiislamu Tanzania (Bamakita) limelitaka Bunge Maalumu la Katiba lijitathmini kama lina ulazima wa kuendelea wakati hakuna uhakika wa kupatikana kwa theluthi mbili ya wajumbe kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kupitisha rasimu ya katiba mpya katika Bunge hilo.

Mwenyekiti wa Bamakita, Sheikh Athuman Mkambaku, amesema wajumbe wa bunge maalumu la katiba hawanabudi kuweka mbele maslahi ya taifa kuliko maslahi ya vyama au kikundi cha watu Fulani.

Shiekh Mkambaku amesema kitendo cha wajumbe wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuendelea kususia vikao vya Bunge hilo si kitendo cha busara kwani msimamo huo unatia shaka juu ya matarajio mema ya Watanzania ya kupata katiba mpya.

Pia amewaomba  watanzania kuuchukua ushauri wa Rais Jakaya Kikwete na kwamba, alichokisema katika hotuba yake ni ushauri, mwongozo na maoni yake kama kiongozi mkuu wa nchi, ambaye ana uwezo huo na kwamba, siyo lazima kwa wajumbe kufuata maoni yake.

Monday, August 11, 2014

MPIGA PICHA WA MIHADHARA YA KIISLAMU ZANZIBAR, MBARONI!



Jeshi la Polisi Zanzibar leo limemkamata mpigapicha maarufu wakujitegemea anayefanya shooting katika mihadhara mbali mbali yakiislam na makongamano na mikutano yakisiasa al-ustadh Salim Khatib.

Akizungumza na waandishi wa habari visiwani zanzibar mlezi wa harakati ya Jumuiya na Taasisi za kiislam Zanzibar samahatu sheikh Haji Khamis Hajji amesema, Mpiga picha huyo amekamatwa mara baada yakumaliza majukumu yake ya kupigapicha katika mkutano wa hadhara wa chama cha upinzani cha National Reconstruction Alliance NRA uliofanyika katika viwanja vya komba wapya mjini Zanzibar.

Aidha amiri Hajji amebainisha kuwa hapo nyuma ndugu Salim aliwahi kuitwa polisi nakuhojiwa kutokana na harakati zake anazozifanya.

Mpigapicha huyo anaeishi maeneo ya makondeko wilaya ya magharibi Unguja na anakisiwa kuwa na umri wa kati ya miaka 35 hadi 40.